Kile Biblia inachofundisha kuhusu msamaha na mwanzo mpya

Inaweza kuonekana kuwa hiawezekani kusamehe, haswa wakati majeraha ni ya kina sana.

Iwe kusamehe mtu mwingine, kujisamehe mwenyewe, au hata kuamini kwamba Mungu anaweza kukusamehe, uzito wa hatia na majuto mara nyingi hudumu kwa muda mrefu kuliko ambavyo tungependa.

Katika ulimwengu unaodai ukamilifu lakini unatoa neema kidogo, Biblia inafichua ukweli muhimu: kwamba msamaha sio tu amri ya Mungu—ni zawadi. Na pamoja na hayo huja ahadi ya mwanzo mpya.

Kwa hivyo, Maandiko yanasemaje kuhusu kuanza upya?

Biblia inasimulia hadithi ya watu ambao walishindwa, walilegea, na kupungukiwa. Hata hivyo walipata ukombozi. Mara nyingi, kwa njia inayovutia sana.

Lakini habari njema kuliko zote ni kwamba, kupitia Kristo, njia hii ya uponyaji na urejeshwaji si tu kwamba inawezekana…imeahidiwa.

Haijalishi ni nini kinachotusumbua maishani—iwe tunatafuta uhuru kutoka katika makosa ya zamani au tunatamani kujenga upya mahusiano yaliyovunjika—msamaha wa kweli wa kibiblia hufungua mlango wa mabadiliko na mwanzo mpya.

Katika makala hii, utagundua:

Je, uko tayari kupata uhuru na kufanywa upya? Hebu tuchunguze kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu msamaha na jinsi inavyoweza kukuongoza kwenye mwanzo mpya kabisa.

Jinsi msamaha wa kweli unavyoonekana kulingana na Biblia

Msamaha wa kweli unahusisha kuachilia. Kwa hiyo msamaha unamaanisha kuchagua uhuru.

Biblia inafundisha kwamba kusamehe ni tendo la kiungu na mazoea ya kila siku.

Ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia chuki na kusalimisha haki ya kulipiza kisasi.

Hii inafanya kazi kwa sababu tendo la kweli la kusamehe halitokani na hisia. Tunafanya hivi kulingana neema ya Mungu, onyesho la upendo Wake usio na masharti, ambao Ametupa sisi sote bure.

Katika Mathayo 18:21-22, Petro alipomuuliza Yesu, “Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?” Yesu akamwambia, “Sikwambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini” (NKJV).

Ili kuwa wazi, 70×7 haikukusudiwa kuwa namba halisi kana kwamba tunatengeneza chati au orodha. Badala yake, Yesu alikuwa anaweka sawa jambo fulani. Huu ulikuwa ni mwaliko Wake mkuu wa msamaha usio na kikomo. Katika kuutoa na kuupokea.

Lakini tunaweza kukumbuka kwamba hili halimaanishi kukataa kosa au kupunguza maumivu. Hapana. Hii inahusu kumruhusu Mungu kuleta uponyaji wa kihisia mahali palipokuwa na uchungu. Tunaposamehe, tunarudia sala ya Bwana,

“Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu” (Mathayo 6:12, NKJV).

Kwa hiyo msamaha sio udhaifu. Kwa hakika, ni nguvu—iliyofungwa katika neema, inayowezeshwa na mfano wa Kristo, wenye nanga katika upendo Wake.

Hebu tuone namna Bwana anavyoitikia tunapoleta majuto na kushindwa kwetu Kwake.

Namna Mungu anavyokabili kushindwa kwetu—na kwa nini rehema zake zina nguvu zaidi kuliko masumbuko yetu

Msamaha wa Mungu haununuliwi. Hutolewa bure.

Agano Jipya limejaa visa vya watu wasio wakamilifu waliopewa mwanzo mpya.

Fikiria mwana mpotevu ( Luka 15 ), ambaye aliacha familia yake katika kuendea mambo ya kibinafsi lakini akakaribishwa tena na Baba ambaye alikuwa na haki ya kumkataa. Au Petro, aliyemkana Yesu Kristo mara tatu…lakini baadaye alirejeshwa na kisha akawekwa na Mungu Mwenyewe kuwa kiongozi katika kanisa la kwanza.

Biblia inasema katika 1 Yohana 1:9:

“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (NKJV).

Hii ina maana kwamba msamaha wa Mungu hauzuiliwi kamwe tunapotubu. Kushindwa kwetu kunaweza kuonekana kama mwisho wa mambo, lakini katika Kristo, siyo mwisho wa Mambo.

Bwana alipomsamehe Daudi baada ya kushindwa kwake kwa kiasi kikubwa kimaadili, haikuwa kuipa udhuru dhambi yake bali kuugeuza moyo wake.

Na iliwezekana.

Rehema hizo hizo hutufikia mimi na wewe leo, kwa sababu msamaha hufungua minyororo ya hatia na aibu ambayo inatuzuia kuishi kikamilifu.

Haijalishi yeyote kati yetu ameanguka kiasi gani, rehema za Mungu zinafika mbali zaidi. Historia yako siyo kauli ya mwisho. Bali Kristo.

Na ili kutukumbusha kwamba hatuko peke yetu katika hitaji letu la rehema, Maandiko yamejaa na watu waliojikwaa, walioanguka, waliokengeuka … au mbaya zaidi. Na bado visa vyao vinaweza kutumika kama kioo—hata ramani ya barabara—kwa ajili yetu.

Visa halisi vya mwanzo mpya katika Maandiko

Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kurejesha. Hapo ndipo tunapomwona Mungu akichukua kile kilichovunjika na kukifanya kuwa kizima tena.

Hapa kuna mifano michache yenye nguvu:

  • Paulo: Akiwa mtesi wa wafuasi wa Kristo, akawa mwinjilisti wa Kikristo mwenye uwezo mkubwa zaidi katika Agano Jipya (Matendo 9). Mwanzo wake mpya ulichochewa na msamaha wa Mungu na wito kwa ajili ya kazi kubwa zaidi.
  • Rahabu: Mwanamke aliyekuwa na maisha yasiyofaa zamani alipata neema na akapewa nafasi ya kuonyesha ujasiri na imani yake katika Mungu alipowalinda wapelelezi wa Kiisraeli. Kisa chake kifupi kina nguvu sana kiasi kwamba alikuwa mmoja wa wanawake watano tu waliotajwa katika nasaba iliyochapishwa ya Yesu (Mathayo 1:5).
  • Mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi: Katika Yohana 8, Yesu alisema, “Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (NKJV). Hakupuuza historia yake-Alimpa mwanzo mpya. Badiliko. Njia ya Wokovu.

Habari hizi siyo visa tu vya kale. Huonyesha kile ambacho Mungu anataka kufanya katika maisha yetu sote. Katika maisha yako! Anataka kubadilisha uchungu na kuvunjika moyo kuwa uponyaji, badala ya aibu, neema, na badala ya majuto, kusudi jipya.

Kila kisa cha msamaha katika Biblia huelekeza kwa Yesu Kristo—mfano mkuu, ambaye alikuja kuishi kati yetu siyo ili atuhukumu, bali aweze kutuokoa (Yohana 3:16-17).

Lakini vipi kuhusu nyakati ambazo sisi ndio tumeumizwa?

Vipi kuhusu nyakati ambazo tumetendewa isivyo haki, tumeachwa, au tumedhulumiwa…na mkosaji hajuti?

Biblia inatufundisha ukweli muhimu kwamba, kwa kuwa tumesamehewa tunaitwa kusamehe. Na ingawa si rahisi, kuna hatua halisi tunazoweza kuchukua ili kusonga mbele kwa neema—na kupata uhuru wa kweli kutoka katika mizigo hii.

Vidokezo muhimu katika kutusaidia kusamehe—hata inapoonekana kuwa haiwezekani

Kuwasamehe wengine ni ngumu sana, haswa ikiwa jeraha ni kubwa. Lakini kazi ya msamaha kamwe siyo kufuta makosa. Badala yake, ni kuchagua uhuru badala ya uchungu na uponyaji wa kihisia badala ya kulipiza kisasi.

(Kwa sababu uchungu na kisasi havijawahi kuleta uponyaji au kutosheka.)

Hapa kuna hatua za kibiblia na halisi:

  • Tambua kwamba msamaha ni uchaguzi, siyo hisia. “Mkichukuliana na kusameheana….kama Bwana alivyowasamehe ninyi” (Wakolosai 3:13, NKJV).
  • Waombee waliokuumiza. Hii haimaanishi kukubaliana nao—inamaanisha kukabidhi maumivu kwa Mungu na kuyaacha mikononi Mwake.
  • Weka mipaka inayoeleweka. Msamaha haimaanishi kuruhusu madhara yajirudie. Hiyo ni dhana potofu kabisa. Badala yake, humaanisha kuwa unasonga mbele kwa hekima (Mithali 4:23).
  • Jikumbushe msamaha ambao Bwana anakupatia. Bwana ametusamehe sisi sote tulipokuwa katika hali mbaya kabisa . Je, utawaonyesha wengine neema hiyo hiyo? (Ona Mathayo 18:23-35.)
  • Rudia mchakato. Wakati mwingine utahitaji kumsamehe mtu yule yule mara nyingi. Unakumbuka saba mara sabini? Ingawa kiwango hiki kinaweza kukukatisha tamaa, haimaanishi kwamba Mungu hayuko kazini.

Kuwasamehe wengine kunakuruhusu kusonga mbele, lakini maneno ya kawaida “samehe na sahau” sio sahihi linapokuja swala la msamaha wa kweli, wa kibiblia. Sio kusahau hata kidogo. Badala yake, ni kukataa mambo yaliyopita kuamua mambo yajayo.

Msamaha huanzisha safari mpya.

Lakini tunaanzaje tena kwa imani, kwa matumaini, na bila uchungu? Hebu tuangalie jinsi ya kutembea kwa ujasiri katika mwanzo mpya ambao Mungu amekuandalia.

Hatua unazoweza kuchukua leo ili kukumbatia mwanzo mpya

Two ears of a sprouting seedling thriving in the new environment.

Image by Pexels from Pixabay

Msamaha ni mlango, na kusonga mbele ni safari. Mara tu unapopokea msamaha kutoka kwa Mungu au kuuonyesha kwa mtu mwingine, hatua inayofuata ni kutembea kwa ujasiri kwenye njia yako mpya na iliyoboreshwa. Hapa unaweza kufanya yafuatayo:

  • Tumia muda katika Maandiko. Acha aya za Biblia zinazohusu msamaha kama Zaburi 103:12 na Waefeso 4:32 kukazia ukweli katika moyo wako.
  • Uwe karibu na jamii. Usitembee safari hii peke yako. Tafuta kutiwa moyo na uwajibikaji kutoka kwa waumini wengine.
  • Badilisha uchungu na shukrani. Weka nakala ya jinsi Mungu anavyokuponya siku baada ya siku.
  • Zingatia utambulisho wako katika Kristo. Hutambulishwi kwa kile ulichotenda, au ulichotendewa. La—unatambulishwa na safari yako, kwa kusonga mbele kwako, na kwa kile Yesu Kristo alichokutendea.
  • Piga hatua za vitendo. Je, kuna mtu unayepaswa kumpigia simu, barua unayopaswa kuandika, au sala unayopaswa kutoa? Hata kama hauko tayari kwa mawasiliano ya moja kwa moja, unaweza kutuma barua ya msamaha.

Safari yako ya uponyaji huanza na uamuzi mmoja: kusamehe na kusonga mbele katika uhuru ambao Yesu pekee anaweza kutoa.

Msamaha sio mwisho-ni mwanzo

Hata hivyo, Biblia haitualiki tu kusamehe. Pia inatuonyesha namna tunavyoweza kusamehe.

Tunaweza kumkumbuka Yesu, Mwokozi wetu, akining’inia msalabani, akimsamehe kila mwanadamu—hata wale ambao wakati huo walikuwa wakimwua na kumchukia. Tunaweza kukumbuka maisha ya watu wasio hesabika katika Biblia waliokombolewa kwa neema. Na kupitia visa vyao, tunaweza kujifunza jinsi ya kuandika visa vyetu.

Tunaalikwa katika hadithi ya matumaini.

Ikiwa umekuwa na hatia, maumivu, au kinyongo, jua hili: Msamaha ambao Mungu hutoa ni wa kweli. Tayari umeshatolewa kwa ajili yako. Na kupitia Kristo, unaweza kukumbatia mwanzo mpya uliojaa kusudi, uponyaji, na amani.

Je, ungependa kujifunza zaidi kuhusu kuishi maisha yaliyojaa neema?

Pin It on Pinterest

Share This