Nini kusudi la Mungu maishani mwangu?
Je, umewahi kusimama katikati ya siku yenye shughuli nyingi na kujiuliza, “Je niliumbwa kwa ajili ya hili?”
Iwe unajiendeleza kitaaluma, unalea familia, unatafuta fursa yako inayofuata, au unajaribu kuelewa misukosuko ya maisha—swali hili hujirudia katika mioyo ya watu wengi.
Ikiwa ndivyo ilivyo, hauko peke yako. Hata watu ambao wanaonekana kuwa na kila kitu mara nyingi husumbuliwa na maswali haya kuhusu kusudi la maisha ndani yao. Shauku ya kuelewa kwa nini tuko hapa—na namna Mungu anavyoweza kutumia maisha yetu—ni mojawapo ya matamanio ya kina ya mwanadamu ulimwenguni.
Uwe kijana anayetafuta mwelekeo, mzazi anayetafuta kuongoza familia yako kwa hekima, au mtaalamu anayetafuta maana zaidi kuliko mafanikio katika usimamizi au mafanikio ya kifedha, makala hii itakusaidia kujiunganisha na kusudi la Mungu aliloliweka ndani yako.
Hebu tujadili Biblia isemavyo kuhusu kusudi la Mungu kwa maisha yako na linavyohusiana na maamuzi yako ya kila siku.
Tutajifunza:
- Kile Biblia inachofunua kuhusu makusudi ya Mungu ya jumla na mahususi kwa kila mmoja wetu.
- Namna ya kutambua wito wako wa kipekee hata katika ulimwengu wenye kelele na kasi.
- Kwanini uko katika hali uliyopo sasa—haijalishi ni ya kawaida au uko katika changamoto—haitaharibu mpango mkubwa wa Mungu.
- Hatua rahisi na zinazofaa ili kuanza kutembea katika kusudi la Mungu kwa uwazi na amani.
Hebu tuanze kwa kuitazama Biblia.
Kile Biblia isemacho kuhusu kusudi la Mungu kwa maisha yako

Photo by Oladimeji Ajegbile
Tunapouliza, “Kusudi la Mungu kwa maisha yangu ni nini?” tunagusa katika mojawapo ya maswali ya kale zaidi na ya kina sana ya kiroho.
Kulingana na Biblia, wanadamu waliumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo 1:27 ), si kwa bahati mbaya, bali kwa kusudi la kiungu na takatifu. Tuliumbwa kuakisi tabia ya Mungu ya upendo na uumbaji, kuishi katika uhusiano Naye, na kutumika kama mawakili wa uumbaji Wake duniani.
Mpango wa Mungu ni zaidi ya kile unachofanya. Bali ni kuhusu umekusudiwa kuwa nani, na kutafuta kufurahia “vitu vidogo” njiani.
Biblia inafundisha kwamba kusudi kuu la Mungu ni kuwaleta watu katika uhusiano wa upendo, wa ukombozi kupitia Yesu Kristo. Warumi 8:28 inatuhakikishia kwamba “katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Tangu mwanzo, mpango wa Mungu kwa wanadamu ulijikita katika upendo, neema, na ukamilifu wa kiroho. Katika safari ya maisha, kusudi la Mungu hufunuliwa kipekee kwa kila mtu, huku siku zote likiendana na maadili ya ufalme Wake yaani: upendo, imani, unyenyekevu, huruma, na haki.
Lakini tunawezaje kuanza kutambua mwelekeo huo wa kiungu katikati ya machafuko yote na vikengeusha-fikira vya maisha ya kila siku? Hebu tuangalie kwa karibu.
Namna ya kutambua wito wako wa kipekee katika ulimwengu wenye kelele na kasi
Kutambua kusudi ambalo Mungu amekupa katika ulimwengu huu linaweza kuonekana kuwa jambo gumu. Kelele za mafanikio, matarajio ya jamii, na usumbufu wa kidijitali mara nyingi huzima kile ambacho Mungu anatuambia.
Lakini hata hivyo, kusudi la Mungu halijafichwa. Linafunuliwa kwa urahisi kupitia Neno Lake, maombi, na mara nyingi kupitia shauku na karama Alizoweka moyoni mwako.
Anza kwa kujiuliza: Je ni nini huniletea furaha, huakisi upendo wa Kristo, na kuwatumikia wengine?
Wito wako mara nyingi hulingana na ambapo furaha yako ya kina hufikia moja au zaidi ya mahitaji ya ulimwengu.
Mungu hawaiti tu wachungaji au wamisionari kushiriki Injili yake ya upendo kwa njia ya kuhubiri. Anawaita walimu, wazazi, wasanii, madaktari, waandishi, mameneja, wasaidizi, wapenda burudani …orodha haina kikomo. Kazi yako inaleta tofauti kwa Mungu inapofanywa kwa upendo, kwa moyo uliojisalimisha Kwake. Wakolosai 3:23 inatukumbusha “Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,” (NKJV).
Hukuumbwa bila mpangilio. Uliundwa ukiwa na karama maalum na njia za kipekee unazoweza kuziendea. Kadiri ufahamu wako wa uwepo wa Mungu unavyokua, ndivyo utakavyoelewa zaidi anavyotaka uishi na kumtumikia.
Bado, unaweza kujiuliza-vipi ikiwa msimu wangu wa sasa hauonekani kama unalingana na mpango wowote mkuu?
Kwa nini yale unayopitia sasa ni sehemu ya mpango mkuu wa Mungu

Photo by Aziz Acharki on Unsplash
Inaweza kuwa vigumu kuona kusudi katika maumivu au uwazi katika machafuko. Lakini Mungu kamwe hapotezi wakati.
Iwe uko “juu ya mlima” au “bondeni,” Yeye anasuka kila kipengele cha maisha yako kuwa na maana kwa umilele. Kama vile Mhubiri 3:1 inavyosema, “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” (NKJV).
Kazi yako, mahusiano yako, hata mapambano yako—yote yanaweza kuchangia jinsi Mungu anavyo kutengeneza kwa ajili ya kazi Yake. Maisha ya Yusufu katika Mwanzo ni mfano wenye nguvu. Alisalitiwa na ndugu zake, kuuzwa utumwani, kufungwa kwa kusingiziwa—lakini mwishowe, Yusufu aliwaambia, “Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia kuwa mema” (Mwanzo 50:20, NKJV).
Hii inatuonyesha kwamba kusudi la Mungu haliko katika hali mambo makamilifu tu. Ubinadamu una uchaguzi wa hiari, ikimaanisha kwamba watu watafanya maamuzi mabaya ambayo yanaweza pia kuwadhuru wengine. Lakini Mungu hataruhusu kamwe uhalisia wa dunia yenye dhambi kumzuia kufanya kazi kupitia wewe. Kusudi lako limefungwa katika maisha yako ya kila siku na mambo yasiyotarajiwa. Amini kwamba hata sasa, Anatumia maisha yako kuakisi upendo Wake, kukuza imani yako, na kuendeleza ufalme Wake.
Kwa hivyo, unaanzaje kuchukua hatua za makusudi kuelekea kusudi hilo? Hapa kuna baadhi ya njia unazoweza kuzitumia kuanza.
Hatua rahisi na halisi za kutembea katika kusudi la Mungu
Kutembea katika kusudi la Mungu hakuhitaji ukamilifu, bali kunahitaji mwelekeo. Hapa kuna baadhi ya njia unazoweza kuzitumia kuanza kupatana na wito wako uliopewa na Mungu:
- Tumia muda katika Biblia – Maandiko yanafunua tabia ya Mungu, matakwa yake kwa wanadamu, na njia mahususi tunazopaswa kuishi na kupenda.
- Omba upate uwazi – Muombe Mungu afunue mapenzi yake. Maombi huimarisha uhusiano wako Naye na kukuza moyo na akili yako ili kutambua vyema ushawishi na uwepo Wake.
- Watumikie wengine – Kusudi mara nyingi hujitokeza unapoanza kupenda watu kwa kujitoa kafara, kama Yesu alivyofanya. Na huduma ya aina hii si lazima ijumuishe ishara kubwa na nzuri. Unaweza kuanza kidogo kidogo, kama vile kumsaidia mtu kubeba vitu hadi kwenye gari lake, kuokota takataka zilizoachwa kwenye bustani, au kujitolea mara moja kwa wiki katika aina fulani ya huduma ya jamii.
- Jihusishe na kanisa – Jamii huimarisha imani yako, hukuwajibisha na kukusaidia, na kukuwezesha kukua kiroho.
- Tafakari na shajara – Kuandika husaidia kufafanua mawazo yako na kufunua namna Mungu anavyokuongoza.
- Uwe tayari kubadilika – Wakati mwingine njia ya Mungu haijanyooka. Amini wakati Wake na neema, hata wakati njia haiko wazi.
Na tukumbuke kwamba kusudi sio kitu “unachokifikia”. Linakuzwa na kutunzwa njiani. Ni mchakato, safari, uvumbuzi. Ni kuwa kama Kristo, Katika namna ya kipekee ambayo ni wewe tu unayeweza.
Uliumbwa kwa sababu
Kila mwanadamu ana kusudi la kiungu. Mungu alikuumba kwa makusudi, kwa upendo, na kwa mpango ambao ni zaidi ya vile ulimwengu unavyoona. Maisha yako ni muhimu, kazi yako ni muhimu, na safari yako ya imani ni muhimu (Waefeso 1:11).
Unapokua katika neema, kuishi katika upendo, na kufuata njia ambayo Mungu anakuangazia mbele yako, utapata aina ya utimilifu wa kiroho ambao hauwezi kupimwa katika hali ya kibinadamu au mafanikio. Ni amani inayotokana na kuishi pamoja na Muumba wako.
Je, ungependa kuendelea kujifunza kuhusu kusudi lako?