Nawezaje Kuacha Kuhisi Hatia kwa Makosa Yangu ya Zamani?

Sote tumewahi kufika hapo—tukiwa tunasumbuliwa na mambo tuliyofanya zamani, namna tulivyoitikia, au maamuzi ambayo tungetamani kuyafuta.

Iwe ni uhusiano tuliouharibu, tabia tunazojutia, au maneno tuliyoyasema na hatuwezi kuyafuta… hatia inaweza kuwa mzigo mzito akilini mwetu. Inabaki ikining’inia, mara nyingi ikipotosha namna tunavyojiona sisi wenyewe na hata namna tunavyoamini Mungu anatutazama.

Wengine huuliza, “Je ni lazima tuhisi hatia yote kwanza ili toba iwe ya kweli?”

Wengine huuliza: Je, kuendelea kubeba hatia si kunatufanya tukae tumekwama kwenye yaliyopita?

Iwapo umechoka kubeba mzigo wa yaliyopita, ni wakati wa kuchunguza hatia kwa mtazamo wa Kibiblia na kutafuta hatua halisi za kuhamia kutoka kujutia hadi uponyaji.

Utagundua:

Tuchunguze jinsi Maandiko yanavyotuongoza kutoka kwenye hatia hadi neema, na kuingia katika maisha yaliyojaa amani, kusudi, na mwanzo mpya.

Tofauti kati ya huzuni ya kiungu na hatia isiyokuwa na faida

A woman praying after studying scriptures to know Bible's teachings on how to with past mistakes.

Image by Gerd Altmann

Kila mtu hufanya makosa, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kuyashughulikia kwa njia yenye afya.
Hatia, ikiwa haishughulikiwi, inaweza kugeuka kuwa mzunguko wa uharibifu unaoharibu kujiamini kwako, afya yako ya akili, na ukuaji wako wa kiroho.

Lakini hatia si zote sawa.Kulingana na Maandiko, kuna tofauti kubwa kati ya huzuni ya kiungu na hatia hatarishi.

“Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.” (2 Wakorintho 7:10, NKJV)

Huzuni ya kiungu inatambua makosa na hupelekea toba (tamaa ya kubadilika) kisha mabadiliko (mchakato wa kubadilika). Inahamasisha mabadiliko mema, huendeleza unyenyekevu, na inatuleta karibu zaidi na Mungu.

Kinyume chake, hatia isiyokuwa na faida au hatia hatarishi mara nyingi hutokana na matarajio yasiyo halisi, kujilaumu, na mazungumzo mabaya ya ndani. Inatufunga kwenye mzunguko wa ukosoaji binafsi na aibu ambao haupeleki kwenye uponyaji.

Iwapo unajikuta mara kwa mara ukijihisi na hatia, ukirudia makosa ya zamani, au ukiwa na mawazo yanayokuletea hatia ambayo hayakuamshi kufanya mambo mema, huenda unakabiliwa na aina ya pili. Kutambua tofauti hii ni hatua ya kwanza kuelekea uponyaji na kusonga mbele.

Lakini tunapaswa kuanzia wapi sasa? Kuelewa hatia ni jambo moja, lakini kushughulikia mzigo wake wa kihisia ni jambo jingine. Tuchunguze jinsi Biblia inavyotufundisha kujibu makosa ya zamani.

Biblia inatufundisha jinsi ya kukabiliana na makosa tuliofanya zamani

Biblia inatoa mwongozo wa jinsi ya kushughulikia hatia na aibu.

Kiini cha mafundisho haya ni ukweli wa msamaha wa Mungu.

“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9, NKJV).

Msamaha huu wa kiungu hautegemei hisia zetu, bali unaegemezwa kwa ahadi za Mungu ambazo hazibadiliki.

Mungu hataki tuwe tumekumbwa na aibu au tujihisi hatufai kwa upendo wake wa kutuponya. Hiyo inapingana na mpango wake wa wokovu. (2 Petro 3:9)

Hivyo, ili kushinda hisia za hatia, wacha tufikirie kuhusu mchakato huu:

  1. Tambua matendo yetu na madhara yake
  2. Tambua haya hadharani mbele za Mungu (kukiri dhambi)
  3. Kubali tamaa ya kubadilika (toba)
  4. Kubali msamaha wa Mungu na mapenzi Yake ya kutuponya

Kushikilia hatia baada ya hatua hii, sio ishara ya unyenyekevu. Badala yake, inakuwa ni kukataa neema ya Mungu.

Mungu hataki tuendelee kukaa katika hisia potovu za zamani zetu bali tubadilishwe kwa kufanywa upya akili zetu (Warumi 12:2).

Pia lazima tujifunze kutambua na kukataa mifumo inayoharibu nafsi, na kujifunza kubadili mawazo yanayokuza hatia na maneno ya Biblia. Mistari kama Warumi 8:1,

Kwa mfano:

“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” (Warumi 8:1, NKJV).

Aya hii inapingana moja kwa moja na imani kwamba lazima tuendelee kubeba hatia yetu kila wakati.

Sasa, wacha tuchambue hatua halisi unazoweza kuchukua ili kuondoa aibu na kuanza kupona.

Njia halisi za kuondoa aibu na kukubali msamaha wa Mungu

Aibu mara nyingi hubaki hata baada ya kusamehewa. Ili kushughulikia aibu hiyo inayobaki, ni muhimu kushiriki kikamilifu katika mambo yanayo thibitisha utambulisho wetu mpya katika Kristo.

Unaweza fanya hivi:

  1. Jifunze kuwa na huruma kwa nafsi yako: Jipatie neema ile ile ambayo Mungu anakupa. Hii inajumuisha kuzungumza kwa wema juu yako mwenyewe na kuepuka mazungumzo mabaya ndani yako.
  2. Jihusishe na tafakari ya nafsi, si kukasirishwa na nafsi yako: Tambua kilichosababisha makosa yako ya zamani na tumia kama uzoefu wa kujifunza.
  3. Pingana na mawazo yanayokuza hatia: Wakati mawazo kuhusu yaliyopita yanapojitokeza, jiulize, “Je, wazo hili linanipeleka kwenye uponyaji au linanifanya nibaki nimeshikilia?”
  4. Weka viwango vinavyowezekana: Acha kujishikilia kwa matarajio yasiyo halisi. Kristo peke yake ndiye mkamilifu. Jukumu letu ni kukua katika Yeye kila siku.

Kuweka mipaka kwa mazungumzo au mazingira yanayokufanya ujihisi na hatia kila wakati kunaweza pia kulinda hisia zako.

Unapofuata kanuni hizi, unaanza kujisikia huru kutokana na mzigo wa aibu uliokuwa nao.

Lakini tunawezaje kuendelea mbele, wakati mambo ya nyuma yanapojaribu kuturudisha tulipotoka?

Kwa nini utambulisho wako ndani ya Kristo ni wa maana kuliko historia yako

Silhouette of crosses at dusk representing a new identity in Christ Jesus.

Image by Gerd Altmann from Pixabay

Kama waumini, utambulisho wetu hauamuliwi na makosa yetu ya zamani, bali na uhusiano wetu na Kristo.

Biblia inasema wewe ni kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Hii inakupa nguvu kusema ‘hapana’ kwa uongo wa hatia unaosema: “Wewe ni makosa yako.”

Hapana.

Kuelewa wewe ni nani katika Kristo husaidia:

  • Kukataa dhana ya hatia na kukubali utambulisho wako kama mtu aliye samehewa na kurejeshwa.
  • Kuacha kujikosoa na badala yake kujiambia kweli: “Ninapendwa. Nimechaguliwa. Nina thamani. Nimesamehewa.
  • Acha kuhisi hatia kwa makosa ambayo Mungu tayari ameyafuta.

Unapokubali utambulisho huu mpya, hatia haikushikilii tena. Sasa unatembea mbele ukiwa na ujasiri katika neema ya Mungu.

Lakini si rahisi kufanya hivi peke yako kila wakati. Hapa ndipo unahitaji faraja na msaada.

Faraja na maneno ya Biblia yatakayo kusaidia kuishi huru

Kujua au kutambua jambo ndilo hatua ya kwanza. Hivyo, uponyaji wa kutoka kwenye hatia hauishii tu kwa kutambua; unahusisha mabadiliko. Mungu hutoa msaada endelevu kupitia Neno Lake, Roho Wake, na watu Wake.

Hapa kuna zana kadhaa za kusaidia safari yako:

  • Kukariri Maandiko: Aya kama Zaburi 86:5, Zaburi 103:12, Isaya 1:18, na Waebrania 8:12 hutukumbusha msamaha kamili wa Mungu.
  • Msaada wa jamii: Jizunguke na watu wanao thibitisha neema na ukweli.
  • Msaada wa kitaalamu: Mshauri wa Kikristo anaweza kukusaidia kufungua hatia kuu, kupitia safari yako ya kihisia, na kuunda mikakati ya kujijali.
  • Kuchukua hatua mwafaka: Fanya marekebisho ikiwa ni lazima na ikiwezekana, kisha endelea mbele. Kudhibiti hatia mara nyingi kunahitaji kufanya marekebisho kama sehemu ya mchakato wa uponyaji – hata kama ni kufanya marekebisho na wewe mwenyewe.

Kama unahisi hatia mara kwa mara, usibebe mzigo huo peke yako. Kutafuta msaada, hata kutoka kwa mtaalamu, ni hatua ya ujasiri na ya kibiblia kuelekea ukamilifu.”

Ingia kwenye uhuru: Safari ina anza sasa

Hatia, unapoiweka mikononi mwa Mungu, inaweza kuwa mlango wa ukuaji, huruma, na kusudi jipya maishani.

Yaliyopita hayakuamulii. Ukiwa na Kristo, unaweza kuishi maisha yenye maana. Acha ukweli Wake uzime sauti ya hatia na kuibadilisha na furaha, amani, faraja, na uwazi.

Hivyo, jipe moyo. Huu si mwisho wa hadithi yako. Huu ni mwanzo wa sura mpya yenye uponyaji na nguvu.

Ili kuendelea na safari yako ya uponyaji na ukuaji wa kiroho, angalia zaidi maarifa ya kutia moyo katika sehemu yetu ya Imani. Utapata makala zitakazokusaidia kuelewa msamaha wa Mungu na kukuwezesha kuishi kwa neema Yake kila siku.

Hapa kuna baadhi ya vitabu na makala tulizoapishwa mahsusi kukusaidia kuelewa zaidi:

Makala hizi zimejaa faraja za Biblia na hekima ya kukusaidia kushinda hisia za hatia, kukubali kusamehe mwenyewe, na kuishi maisha huru na yenye furaha kama Mungu alivyo kusudia.

Pin It on Pinterest

Share This