Namna ya kumkabidhi Mungu kesho yetu
Kuweka kesho yetu mikononi mwa Mungu linaweza kuonekana kama jambo gumu sana, hasa wakati kuna hali ya kukosa uhakika kabisa.
Hata hivyo, kuweka imani yako katika mpango wa Mungu huleta amani na uhakika, hata wakati njia iliyo mbele yako ni giza.
Biblia imejaa mafundisho yanayotukumbusha kuhusu uaminifu wa Mungu na wakati Wake mkamilifu.
Kwa kujifunza kumwamini Yeye, tunaweza kukabiliana na maisha ya baadaye kwa ujasiri, tukijua kwamba yako mikononi mwa Mungu.
Mafundisho ya Biblia kuhusu kumtegemea Mungu
Biblia imejaa aya na visa vinavyotufundisha kutegemea hekima ya Mungu na kuamini mipango Yake kwa maisha yetu.
Mfano mmoja wenye nguvu unapatikana katika Yeremia 29:11, ambapo Mungu anasema, “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” (NKJV)
Aya hii inatuhakikishia kwamba Mungu ana mpango, hata wakati hatuwezi kuuona.
Mfano mwingine mzuri wa imani ni kisa cha Ibrahimu.
Katika Mwanzo 12, Mungu alimwita Ibrahimu aondoke nyumbani kwake na aende katika nchi mpya, bila kumwambia nchi hiyo ilikuwa wapi. Ibrahimu aliamini ahadi ya Mungu, na kwa sababu ya imani yake, akawa baba wa mataifa mengi.
Safari yake inatukumbusha kwamba kumwamini Mungu mara nyingi humaanisha kuingia katika yasiyojulikana kwa ujasiri kwamba Mungu atatuongoza.
Hatua za kuimarisha imani yako
Kujenga imani katika Mungu kunahitaji muda na juhudi za makusudi.
Hapa kuna baadhi ya hatua unazoweza kuchukua ili kuimarisha imani yako na kutegemea zaidi uongozi wa Mungu kwa ajili ya siku zijazo:
- Omba mara kwa mara: Maombi ni njia ya moja kwa moja ya kuwasiliana na Mungu, ambapo unaweza kumshirikisha matumaini yako, hofu, na wasiwasi kuhusu siku zijazo. Muombe Mungu akupe hekima na mwongozo katika njia ya maisha yako.
- Tafakari Maandiko: Pata muda wa kusoma na kutafakari aya za Biblia zinazosisitiza uaminifu wa Mungu. Aya kama Mithali 3:5-6, inasema, “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;” inatukumbusha kwamba Mungu anajua kilicho bora kwa ajili yetu (NKJV).
- Tafuta uongozi wa Mungu: Unapofanya maamuzi, iwe makubwa au madogo, chukua muda kumuomba Mungu ili akupe mwongozo. Amini kwamba atakuwezesha kuelewa wakati wake, hata wakati majibu hayapatikani kwa mara moja.
As you take these steps, you’ll find that your relationship with God deepens, and trusting Him with your future becomes more natural.
Unapochukua hatua hizi, utagundua kwamba uhusiano wako na Mungu unazidi kuimarika, na kumkabidhi kesho yako inakuwa jambo rahisi.
Kushinda mashaka na hofu
Ni kawaida kuwa na mashaka na hofu tunapofikiria kuhusu siku zijazo.
Mara nyingi tunataka kudhibiti kila kitu, lakini imani ya kweli humaanisha kuachilia udhibiti huo na kuamini kwamba Mungu anajua kilicho bora. Katika Mathayo 6:34, Yesu anatukumbusha “Basi msisumbukie ya kesho, kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe.” NKJV.
Hii inatufundisha kuishi maisha yetu leo na kuamini kwamba Mungu tayari anashughulikia kesho yetu.
Wakati mashaka yanapojitokeza, kumbuka uaminifu wa Mungu katika maisha yako yaliopita.
Fikiria nyakati ulipokuwa ukiomba mwongozo au ulinzi, na Mungu akakupatia. Acha nyakati hizi za uaminifu ziimarishe imani yako katika mipango Yake kwa ajili ya siku zijazo.
Kuachilia na kukumbatia imani
Kuachilia udhibiti na kumwamini Mungu kikamilifu linaweza kuwa ni jambo gumu, lakini ni moja ya hatua za kuwa huru zaidi unazoweza kuchukua katika safari yako ya imani.
Kumbatia imani kwa kumkabidhi Mungu kesho yako, ukijua kwamba mipango Yake ni mikubwa zaidi kuliko chochote unachoweza kufikiria.
Warumi 8:28 inatuhimiza kwa maneno haya:
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” NKJV.
Kwa kukumbatia imani, unachagua kuamini hekima na wema wa Mungu, hata ambapo wakati ujao haujulikani. Kuamini huku hakumaanishi kwamba maisha yatakuwa yasiyo na changamoto, lakini inamaanisha kwamba hautazikabili changamoto hizo peke yako.
Kupata amani katika mpango wa Mungu
Kumkabidhi Mungu kesho yako huleta amani inayozidi ufahamu wa kibinadamu.
Unapomtegemea, unaweza kuwa na uhakika kwamba chochote kitakachokujia, Mungu yuko katika udhibiti.
Isaya 26:3 inahidi kwamba Mungu atawalinda katika amani kamilifu wale wanaomwamini.
Kwa kuimarisha uhusiano wako na Mungu, kutafuta uongozi Wake, na kuachilia hofu zako, unaweza kukabiliana na siku zijazo kwa matumaini, ukijua kwamba Mungu anakuongoza katika kila hatua ya njia.
Kwa mahamasisho zaidi juu ya kukua katika imani na kumwamini Mungu na siku zako zijazo, tembelea kurasa nyingine kuhusu imani kwenye HFA.
Na ili kujifunza zaidi kutoka katika Neno la Mungu, jiandikishe hapa kwa ajili ya masomo ya Biblia mtandaoni bure.
Sehemu inayobaki ya ukurasa huu imekusudia kukutia moyo kwa kuimarisha imani yako katika Yesu. Taarifa ifuatayo inaeleza mtazamo wa kibiblia kuhusu kuwa na tumaini na kumkabidhi Mungu kesho yetu.
Pata mtazamo mwingine kuhusu mada hii kupitia video hii
Tahadhari: Hope for Africa haihusiani na video ifuatayo. Inatolewa tu kama nyenzo muhimu katika kujifunza kukabidhi Mungu kesho yetu.
Somo la 4 || Tumaini la Agano la Kale || Kuhusu Kifo, Kufa, na Tumaini la Baadaye – Hope Channel Kenya
“Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;. . . . akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.”
|| Waebrania 11:17, 19 || NKJV
Aya 8 za Biblia kuhusu kumkabidhi Mungu kesho yetu
Imeandaliwa na wafanyakazi wa Hope For Africa mnamo Septemba 23, 2024
Aya za Biblia kuhusu “Namna ya kumkabidhi Mungu kesho” kutoka Toleo la New King James (NKJV)
- Mithali 3:5-6
“Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”
Maelezo: Tunaweza kumtumaini Mungu kuongoza maisha yetu na siku zetu zijazo.
- Yeremia 29:11
“Maana najua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani na si ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini siku za mwisho.”
Maelezo: Mungu anatuhakikishia kwamba ana mipango mizuri kwa ajili ya siku zetu za usoni, na tunapaswa kuikabili kesho kwa matumaini.
- Wafilipi 1:6
“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”
Maelezo: Aya hii inatupa ujasiri kwamba Mungu atatuongoza katika maisha yetu na kukamilisha kazi nzuri anayofanya ndani yetu.
- Zaburi 37:5
“Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.”
Maelezo: Mipango yoyote tuliyonayo kwa ajili ya siku zijazo, tunatiwa moyo kuiwasilisha mbele za Mungu kwa imani na Yeye atayatekeleza.
- Mathayo 6:34
“Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Maelezo: Badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu kesho na siku zijazo, Yesu anatuita kufikiria kuhusu leo na baraka anazotupatia sasa.
- Zaburi 56:3
“Siku ya hofu yangu nitakutumaini wewe.”
Maelezo: Wakati wowote tunapokuwa na hofu kuhusu kinachokuja mbele yetu, Biblia inatutia moyo kumtegemea Mungu.
- Zaburi 37:23-24
“Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza”
Maelezo: Aya hii inatuonyesha kwamba Mungu anatuongoza katika kila hatua ya maisha yetu tunapomwamini na kumtii.
- Warumi 8:28
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Maelezo: Aya hii inaonyesha kwamba Mungu ana kusudi katika yote yanayotokea katika maisha ya watu Wake, na Yeye hugeuza yote kuwa mema kwa ajili ya watoto Wake.
Tafuta StepBible.org kwa maelezo zaidi kuhusu kumtegemea Mungu.
Mada na aya hukusanywa kutoka katika nyenzo mbalimbali na kupitiwa na timu yetu. Ikiwa mada au aya haifai au haipo, tafadhali wasiliana nasi. Maandiko yamechukuliwa kutoka toleo la New King James Version®. Hakimiliki © 1982 na Thomas Nelson. Imetumika kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa.
Wasiliana nasi
Je, una maswali kuhusu mada hii? Au una mawazo kuhusu mada zijazo? Tungependa kusikia kutoka kwako! Unachopaswa kufanya ni kujaza fomu hapa chini. Timu yetu itakujibu haraka iwezekanavyo.
Changia mawazo yako kuhusu tumaini kwa ajili ya kesho
Hapa ndipo unapata kushiriki katika mazungumzo. Shiriki kwa kuchangia mawazo yako kuhusu kumkabidhi Mungu kesho yetu!
Majadiliano yanaratibiwa. Tafadhali soma Sera Yetu ya Maoni.