Misingi ya Kutuongoza Tunapochagua Marafiki
- Marafiki huathiri maisha yako ya baadaye
Marafiki unaowachagua wanaweza kuwa na athari kubwa kwenye maisha yako ya baadaye. Wanaathiri namna unavyofikiri, maamuzi unayofanya, na aina ya mtu unayekuwa. Chagua marafiki wanaokusaidia kukua, kuepuka matatizo, na kufikia malengo yako.
- Tafuta wale mnaoshiriki maadili sawa
Marafiki wazuri huwa na maadili yanayofanana. Je, wanaamini katika kufanya kilicho sawa? Je, wanawaheshimu wengine? Chagua marafiki wenye misimamo ya kimaadili kama yako na wanaotamani mambo mema kama wewe maishani.
- Uliza maswali sahihi
Njia nzuri ya kujua kama mtu ni rafiki mzuri ni kujiuliza:
Je, ninahisi vipi baada ya kutumia muda naye?
Je, wananisaidia kufanya maamuzi ya busara?
Je, wapo pale ninapohitaji msaada au faraja?
Kama majibu ni ndiyo, basi huenda huyo ni rafiki mzuri
- Ni sawa kujitenga
Kama mtu hakusaidii kukua au anakuelekeza kwenye njia isiyo sahihi, ni sawa kujitenga naye. Kufanya uamuzi sahihi kuhusu marafiki leo kunaweza kukusaidia kufanya maamuzi bora zaidi siku za baadaye.
- Fikiria matokeo ya muda mrefu
Marafiki ulionao sasa wataathiri tabia zako na maamuzi yako ya baadaye. Jizungushe na watu wanaokuinua na kukusaidia kuwa bora, ili uwe na maisha ya baadaye yenye mwanga na mafanikio.
Kuchagua marafiki wenye maadili sawa na yako na kukuhamasisha kukua kutakusaidia kujenga mustakabali mzuri. Unapowaza kuhusu watu katika maisha yako, kumbuka kwamba urafiki mzuri husababisha matokeo mazuri.
Jifunze zaidi kuhusu namna kujenga urafiki imara katika kurasa zetu za mahusiano hapa HFA!
Tazama video kuhusu jinsi ya kuchagua marafiki wazuri
Maelezo ya Video: Hakuna mmoja wetu, ikiwa ni pamoja na wajasiriamali, anayeweza kufanikiwa bila marafiki. Hapa kuna vidokezo vya namna ya kuchagua marafiki wazuri.
Aya 10 za Biblia kuhusu kuchagua marafiki na wendani
Imeandaliwa na wafanyakazi wa Hope For Africa tarehe 19 Septemba, 2024.
Aya za Biblia Kuhusu “uchaguzi wa marafiki na watu wanaotuzunguka” kutoka Tafsiri ya New King James (NKJV).
- Mithali 12:26
“Mwenye haki ni kiongozi cha mwenzake; Bali njia ya wasio haki huwakosesha..”
Maelezo: Mtu anayejali kufanya mambo yaliyo sahihi hachagui tu mtu yeyote kuwa rafiki, bali huchunguza kwa makini na kwa tahadhari ni nani anayefaa kuwa rafiki yake wa karibu. Anaelewa kwamba urafiki na mtu mwenye tabia au mwenendo mbaya unaweza kumuathiri na kumuelekeza kwenye njia isiyo sahihi.
- Mithali 13:20
“Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”
Maelezo: Uchaguzi wa rafiki au mwenza una athari kubwa katika maendeleo ya mtu. Kuwa karibu na watu wenye hekima kunakusaidia kukua katika hekima, kukuza ujuzi sahihi, na kupanua upeo wako wa fikra, lakini kushirikiana na watu wasio na hekima au marafiki wabaya kunakwamisha ukuaji wako na kukuingiza katika matatizo.
- Mithali 17:17
“Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.”
Maelezo: Rafiki wa kweli au mwema na mwenye maadili siku zote huonyesha upendo wa dhati, hata wakati wa shida au dhiki, hujihusisha kana kwamba ni mwana familia. Vilevile, marafiki wa kweli na jamaa wa kweli hupenda katika mafanikio au matatizo, na hakuna hali yoyote itakayowatenganisha na maisha ya rafiki yao.
- Mithali 18:24
“Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.”
Maelezo: Tukichagua kuwa na marafiki, tunapaswa kuendeleza uhusiano huo na kuonyesha kuwa tunawathamini kupitia maneno na matendo yetu ya upendo. Hata hivyo, kuwa na marafiki wengi wasio na busara au wasioaminika kunaweza kuchosha na hawatatuunga mkono nyakati za shida. Lakini rafiki wa kweli na wa maana atasimama nasi kwa uaminifu hata pale ndugu wa damu wanapotugeuka.
- Mithali 27:17
“Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.”
Maelezo: Kama vile chuma hutumika kusugua kisu au panga ili kukinoa na kukitia makali vizuri, vivyo hivyo mazungumzo ya busara na yenye manufaa na watu wenye maarifa humnoa mtu kiakili. Kwa upande mwingine, kushirikiana na watu wenye tabia mbaya pia kunaweza kuunda tabia yetu kwa namna isiyofaa.
- 1 Wakorintho 15:33
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.'”
Maelezo: Hatutakiwi kudanganyika tukidhani kwamba wale tunaoshirikiana nao (iwe ni walimu, marafiki, n.k.) hawana athari kwa tabia zetu. Kinyume chake, watu tunao jihusisha nao wanaweza kuathiri tunavyokuwa na hata kuharibu tabia njema. Kwa hiyo, tunapaswa kuepuka walimu wa uongo na marafiki waovu, na badala yake tuchague watu wa kumcha Mungu kuwa marafiki wa karibu.
- Mithali 22:24-25
“Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.”
Maelezo: Uovu huzaa uovu. Kwa hiyo tunapaswa kuepuka kushirikiana na watu wenye hasira za haraka au wasioweza kujizuia wanapokasirika, kwa sababu kuwa karibu nao kunaweza kutufanya tuwe na tabia kama zao na hatimaye kujiletea maangamizi.
- Mhubiri 4:9-10
“Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!”
Maelezo: Hakuna mtu anayeweza kuishi peke yake, na tamaa ya ubinafsi haina faida ya kweli. Lakini kuwa na jamii, rafiki, au kundi la msaada karibu nawe kuna thamani kubwa zaidi, kwa sababu mnaweza kuimarishana, kutiana moyo, kufarijiana, na kusaidiana wakati wa changamoto au mahitaji.
- Mithali 27:6
“Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.”
Maelezo: Ni bora kuwa na rafiki wa kweli ambaye anaweza kukukosoa kwa upendo na kwa nia njema, kuliko kupokea maneno matamu kutoka kwa mtu anayekuchukia. Ingawa maonyo ya rafiki yanaweza kuumiza mwanzoni, ni ya kuaminika zaidi kuliko busu au ishara za urafiki kutoka kwa adui.
- Yakobo 4:4
“Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.”
Maelezo: Urafiki wa hali ya juu kabisa ni ule kati yetu na Mungu. Kutafuta furaha au kibali kutoka kwa dunia, au kuwa na urafiki na anasa za dunia au mazoea ya dhambi, kunaweza kupotosha akili na mioyo yetu na kutufanya kuwa maadui wa Mungu.
Mada na aya hukusanywa kutoka nyenzo mbalimbali na kupitiwa na timu yetu. Ikiwa aya au mada haifai au haipo, tafadhali wasiliana nasi. Maandiko yamechukuliwa kutoka Toleo la New King James®. Hakimiliki © 1982 na Thomas Nelson. Limetumika kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa.
Wasiliana nasi
Je, una maswali yoyote kuhusu urafiki mzuri au jambo lingine? Au una mapendekezo ya mada za baadaye ambazo ungetamani tuzijadili ? Tafadhali jaza fomu iliyoko hapa chini. Tungependa kusikia kutoka kwako!
Jiunge na mazungumzo kuhusu namna ya kuchagua marafiki wazuri
Je, una maswali zaidi kuhusu namna ya kutengeneza marafiki wazuri? Je, una maoni yeyote kuhusu swala hili? Shiriki nasi katika eneo la maoni hapa chini!
Mijadala inaratibiwa. Tafadhali soma Sera Yetu ya Maoni.