Vijana Sita wa Kiafrika Walioleta Mabadiliko katika Jamii Zao

Watoto barani Afrika wanachochea mabadiliko na kubadilisha jamii—hata nchi nzima. Miongoni mwao kuna wanamichezo mashuhuri, wabunifu, wanaharakati, wataalamu, wakalimani wa lugha, n.k. Vijana hawa wanawatia moyo wengi zaidi kufuata nyayo zao.

Wamethibitisha kuwa changamoto—kama vile kutopata elimu, umaskini, magonjwa,ukosefu wa ajira, na ukosefu wa huduma za kijamii—zinaweza kushindwa, na mitazamo hasi inaweza kubadilishwa.

Katika wasilisho, “Hatari ya Hadithi Moja,” tunashauriwa kuhadithia kwa wingi hadithi za Kiafrika.1 Hivyo basi hizi ni hadithi chache za mabadiliko kuhusu vijana bora barani Afrika:

  1. Sadio, mwanasoka mahiri
  2. John aleta umeme kwenye kijiji chake
  3. Juhudi za Ayeshaitu kupata elimu
  4. Maya, mtafsiri mwenye ufanisi wa lugha ya kichina
  5. Noah akuwa mkurugenzi mkuu akiwa na miaka 14
  6. Tanya alikabiliana na kikwazo cha ugonjwa

Sadio kivutio cha soka2

Akianzia katika maisha ya kawaida huko Bambali, kijiji kidogo cha Senegali, upendo wa Sadio Mane kwa soka ulistawi.

Alikulia katika jamii maskini, lakini licha ya rasilimali chache, mchezo wa soka ulikuwa ni kivuli chake cha matumaini. Alijiunga na vilabu vya mitaani na kuanza safari yake kuelekea kuwa mchezaji mtaalamu.

Katika umri wa miaka 15, akiwa amevaa viatu vilivyochakaa na kaptula iliyoshonwa kwa mkono, kipaji chake asili kilionekana wazi wakati wa jaribio muhimu huko Dakar, mji mkuu wa Senegali.

Uchezaji wake wa kuvutia ulikuwa msingi wa safari ya ajabu, kutoka Afrika Magharibi hadi kuwa gwiji wa soka.

Kuingia kwake kwenye ulimwengu wa soka

Kutoka mwambao wa Senegali, Sadio aliwasili Uingereza, lugha ya kingereza ikiwa changamoto lakini kipaji chake kiking’aa bila kikomo.

Kijana huyu aliutawala upande wa kushoto wa klabu ya Liverpool, akiwashangaza watazamaji kwa kasi kama umeme na ustadi wa hali ya juu. Juma moja baada ya jingine, alifunga mabao ya kushangaza, akiwaacha wanahabari wa michezo kwenye mshangao mkubwa.

Ni nani huyu kijana mdogo wa Kiafrika mwenye kipaji cha ajabu? Alikotoka, ilikuwa ni fumbo, lakini hakuna aliyepinga uwezo wake, Sadio akawa jina linalo zungumzwa katika ulimwengu wa soka.

Taaluma ya kuvutia

Liverpool, moja ya klabu kubwa duniani, ilimpata Sadio kama mchezaji wake bora. Talanta yake iliipeleka timu kileleni, ikashinda taji na vikombe vya thamani.
Kwenye uga wa kimataifa, Sadio alikuwa mchezaji muhimu wa Senegali, akitambulika kama mchezaji bora wa timu.

Mchango wake kwa klabu na timu ya taifa ulivuka mipaka, akawa na mchango mkubwa kwa soka ya Uingereza na Afrika. Ametajwa kuwa Mchezaji bora barani

Afrika na pia amekuwa miongoni mwa walioteuliwa kwa Ballon d’Or, tuzo kuu ya soka duniani.

Safari ya Sadio imejenga hadhi yake miongoni mwa wachezaji bora, huku ikiacha alama isiyoweza kufutika katika historia ya soka.

Matokeo ya mafanikio yake

Kutoka kwenye maisha ya kawaida hadi kufikia umaarufu wa soka, safari ya Sadio inatufundisha kutazama zaidi ya vizuizi vinavyoweza kutuzuia.

Na kisha kurudisha kwa jamii baada ya kupata fursa ya kukua. Uwezo wake uwanjani umemletea utajiri, ambao sasa anautumia kuwekeza katika maendeleo ya Senegali kwa siku za zijazo.

Sadio hakusahau asili yake. Ili kuwasaidia wengine kushinda vikwazo vya mazingira yao, ameweza kujenga shule za kusaidia watoto katika kijiji chake, na hospitali ili kupambana na athari mbaya za magonjwa. Miradi hii yote imefadhiliwa na mafanikio yake.3

Wachezaji wadogo wa soka, wakiona mafanikio yake, wanatamani kufuata nyayo zake, kwenye uwanja na pia katika kutoa msaada kwa jamii. Na Sadio siyo kijana pekee aliyeleta mabadiliko katika jamii yake. Mkenya mmoja alikuwa shujaa kwa kuleta umeme katika kijiji chake bila kuwa na elimu ya chuo kikuu.

John aleta umeme kwenye kijiji chake4

Sometimes what we play around with can lead to an incredible journey. John's interest in wires led him to bring light to his people.Katika sehemu za bara ya Kati nchini Kenya, mvulana aitwaye John alipenda kuchezea nyaya. Licha ya kuwa na maisha magumu, alikuwa na shauku kubwa ya kujifunza mambo ya umeme.

Akiwa shule ya msingi, John alikumbana na changamoto kubwa ya kusoma na kuandika.5Lakini ndani yake, kipaji kilicho fichika kilikuwa kinasubiri kuangaza, kutoka maisha ya kijijini hadi ustadi wa kiteknolojia, na hatimaye kuwa mhandisi wa umeme wa kijiji chake.

Mwanzo wa safari hii

Walimu walimwona John kama “asiyejiweza” kutokana na alama zake duni, na hivyo akaamua kutojiunga na chuo baada ya kumaliza shule ya sekondari. Badala yake, aliamua kufanikisha ndoto yake ya kuzalisha umeme. Watoto wengi kijijini mwao walikumbana na changamoto ya kusoma usiku kwa sababu majumbani mwao hakukuwa na umeme.

Ni wachache tu waliotambua kipaji chake. Aliuza mifugo, akanunua vifaa, na kuwaahidi majirani zake kuwa angewapatia umeme—ambao ulikuwa ghali sana kujiwekea wakati huo nchini Kenya.

Majirani zake hawakumtarajia kufanya lolote la maana. Baadhi walimwona kama kichaa na hata kupendekeza aende kuona daktari wa akili! Hakuna mradi kama huo uliwahi kufanyika katika kijiji chao.

Wengine bado waliamini kuwa alihitaji angalau elimu ya chuo kikuu ili kutimiza ndoto yake. Hata hivyo, shauku yake ilimchochea kuvuka vikwazo na kushangaza wengi.

Kwa kuchagua njia isiyo ya kawaida, John aliwathibitishia waliomdharau kuwa ubunifu unaweza kuzidi elimu ya kawaida.

John ageuka kuwa mhandisi stadi

Azma ya dhati ilimchochea John kufikia ndoto yake ya kuleta umeme kwa kijiji chake.

Bila elimu rasmi, akiwa na maarifa ya fizikia kutoka shule ya sekondari,alikabiliana na changamoto hiyo kwa ujasiri. Aliuza sungura ili kupata fedha za kununua vifaa muhimu.

Matokeo yake? Kiwanda cha nyumbani cha umeme katika maeneo ya mashambani Kenya.

Sasa, wakazi wanapata faida ya umeme wake, hii imeboresha sekta ya nishati ya Kenya. Matokeo yake, shughuli nyingi za uchumi zimefaidika. Wanafunzi sasa wanaweza kuendelea na masomo jioni, na pia maeneo ya burudani yameibuka kijijini.

Ubunifu wa John unang’aa, ukileta mwangaza majumbani na kuwapa motisha wengine.

Ubunifu wake waenea hadi nchi nyingine

Mradi wa John wa kutengeneza umeme kwa kutumia nguvu za maji unatoa mwangaza kwa nyumba 2000, na ni uthibitisho wa bidii yake. Majirani waliomdharau sasa wanapata matunda ya juhudi zake.

Kwa uwepo wa umeme, kijiji chake sasa kimeboresha huduma za afya, elimu, na uzalishaji wa kiuchumi. Huu ni mchango muhimu kwa malengo ya maendeleo endelevu barani Afrika, yaliyowekwa na serikali yake, ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika vijiji vya Afrika.

Jamii nyingine za Kenya zilianza kutumia ubunifu wake, kutokana na njia yake rahisi ya uzalishaji. Baadaye, miradi ya vijijini nchini Ethiopia, Rwanda, na Uganda ilifuata mfano wake.

Ushujaa wa John unadhihirisha kuwa mtu mmoja anaweza kuanzisha mabadiliko. Na wewe pia una uwezo wa kubadilisha maisha.

Kinachofuata ni kisa cha kijana mmoja kutoka Ghana, aliyebuni fursa za kugharimia masomo yake.

Jitihada za Ayeshaitu ya kupata elimu

Ayeshaitu alikuwa yatima akiwa na umri wa miaka sita. Mama yake alifariki alipokuwa na miaka mitano na baba yake alifariki mwaka uliofuata.

Yeye na ndugu zake wakubwa waliishi na mlezi aliyewalea pamoja na yatima wengine. Lakini mlezi huyo hakuwa na kazi, hivyo alihangaika kumudu mahitaji yao ya kila siku.

Akiwa na umri wa miaka 16, umasikini ulimfanya Ayeshaitu asione maisha yake yakiwa na mwangaza. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuolewa akiwa mdogo au kuuza bidhaa mitaani bila kupata faida ya maana.

Aliazimia moyoni mwake kuvunja kizuizi cha umasikini na kujitengenezea njia tofauti. Kwa nia ya kuushinda umasikini uliomzunguka,alichukua jukumu la elimu yake mikononi mwake.

Alikabiliwa na changamoto

Kutokana na ukosefu wa fedha, Ayeshaitu hakuweza kujiunga na shule ya sekondari. Lakini hakuruhusu safari yake ya elimu kuishia pale.

Kwa miaka mitatu alishindwa kufaulu katika mtihani wa kuingia sekondari kwa sababu ya ukosefu wa maandalizi na pesa, Ayeshaitu alizidi kujitahidi. Wakati dada zake walikata tamaa na kuolewa, yeye aliamua kuboresha maisha yake kupitia elimu.

Fursa alizounda ili apate karo ya shule

World Vision, kupitia programu yake ya Cocoa Life, iliwezesha kikundi cha akiba cha wanawake katika kijiji cha Ayeshaitu. Kupitia kikundi hiki, aliweza kujiwekea fedha na kupata msaada wa kulipia masomo yake.

Akitumia fursa hii kugharamia elimu yake, alijiunga na shule licha ya vikwazo vya umri. Azma yake ilimfanya apewe ruhusa maalum ya kuvuka kizuizi cha miaka 18 na zaidi.

Ayeshaitu alielekeza mapato kwenye akiba, kutoka kwa kazi ya kuuza bidhaa mitaani, jambo lililomuwezesha kulipia karo ya shule, mahitaji ya shule, na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadaye.

Mafanikio ya elimu

Ayeshaitu, sasa amerudi shuleni na anajitegemea, anatarajia kujiunga na chuo cha kijeshi. Alifanya vizuri katika mitihani yake ya mwisho na akakubaliwa kujiunga na chuo hicho. Anatumai kufanya kazi katika jeshi baada ya kumaliza mafunzo yake.

Anatumaini pia kukusanya pesa ili aanzishe biashara ndogo kwa ajili ya ndugu zake. Ananuia kuwa stadi wa ushonaji na anapanga kujifunza kutengeneza “mikoba ya Kiafrika.”6Macho yake yanaangaza tumaini anaposema.7“Ninataka kuwatia motisha wasichana kutoka miji midogo wanaopitia changamoto kama nilizopitia… Kwa kujituma, mtu yeyote anaweza kufanikisha mambo makubwa.”

Kifuatacho, Akiwa yatima tangu utotoni, Maya alikabiliana na changamoto za kujifunza lugha ya kigeni na hatimaye akajenga taaluma yenye mafanikio kama mkalimani.

Maya, mkalimani mahiri wa Kichina (Mandarin)

Maya,8mkalimani wa Umoja wa Mataifa anayefanya kazi Nairobi, Kenya, alitenga muda kwa mahojiano ili kusimulia safari yake ya mafanikio. Alianza kwa kusalimia kwa Kichina, “NI HAO MA,” akimaanisha “Habari.”

Haikumchukua muda kuwa mtaalamu wa lugha. Kichina ni lugha ngumu kujifunza hasa kwa sababu kina herufi tofauti na zile za lugha nyingi za Kilatini.

Ingawa anafanya kazi Afrika Mashariki, Maya anatoka Lusaka, Zambia, kusini mwa Afrika. Alikulia katika viunga vya jiji hilo. Mapema maishani mwake, alipata fursa kutoka Afrika hadi Asia, na kuboresha mtazamo wake katika mawasiliano ya kimataifa.

Changamoto za kupoteza wazazi wake akiwa mdogo

Tofauti na watoto wengi wa Zambia, Maya alizaliwa katika familia yenye maisha mazuri ya kipato cha kati. Hata hivyo, maisha yake yalibadilika ghafla alipopoteza wazazi wake katika ajali mbaya akiwa na umri wa miaka mitano.

Tukio hili lilibadilisha maisha yake kabisa. Kwa bahati mbaya, baadhi ya jamaa zake waliopaswa kumtunza walitumia vibaya akiba ya fedha iliyoachwa na wazazi wake. Matokeo yake, Maya alijikuta hana msaada aliouhitaji ili kufanikiwa maishani.

Na kama haitoshi, akiwa na umri mdogo, alidhulumiwa na jamaa zake wa karibu, jambo lililompelekea kufanya uamuzi wa kishujaa wa kuondoka na kutafuta hifadhi katika nyumba ya watoto yatima.

Maya alishinda changamoto ili kuifikia taaluma yake

Kuna wakati, Maya alijiona kama maisha yake yalikuwa yamejaa giza. Ilikuwa vigumu kwake kuona sababu ya kusonga mbele. Hata hivyo, kukutana na wasichana wengine waliokumbana na changamoto kama yake kulimpa moyo kubaki na matumaini.

Alipata nguvu katika imani yake kwa Mungu, aliyatoa maisha yake kwa Yesu na kuhudhuria maombi kila mara kwenye kanisa la mayatima. Wakati wa kujiunga na chuo kikuu ulipofika, Maya alijaliwa kupokea ufadhili wa serikali ya China kwa ajili ya masomo nchini China. Ufadhili huu hutolewa kwa wanafunzi wenye vipaji katika maeneo maalum ya masomo, na Maya alikuwa na kipaji cha lugha.

Maya amekuwa akifaulu shuleni na kuwashangaza watu wengi kwa mafanikio yake. Alihitimu kwa shahada bora zaidi katika Lugha na aliendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamili katika Masomo ya Maendeleo ya Kimataifa. Baada ya kuhitimu, alihamia Nairobi na alikuwa na furaha kuanza kazi yake kama mtafsiri wa lugha.

Maya anawatia moyo wengine kama mtaalamu wa lugha

Kujifunza Kichina na kuwa mtafsiri ina changamoto zake, lakini pia ni safari yenye matokeo mazuri! Maya anajiona kama chombo cha wema, akiwasaidia wengine kwa baraka alizopokea.

Anapenda kuzuru nchi mbalimbali za Afrika na hutumia muda wake wa mapumziko kuhamasisha na kuwapa motisha wengine. Kupitia mitandao ya kijamii, anawasiliana na kuwainua wale walioko katika hali ngumu kwa kuwahadithia kisa chake na kusaidia kuwaunganisha na vyanzo vya ufadhili wa masomo.

Kisha, kutoka Uganda, tunapata kisa mvulana mdogo aliyetengeneza kampuni yake akiwa bado kijana.

Noah alikuwa mkurugenzi mkuu akiwa na miaka 14

Alipokuwa mdogo, Noah Walakira9 alikuwa akiishi na nyanya yake, wakati wa likizo.

Lakini haikuwa tu kusikiliza hadithi za jadi na kupata zawadi kutoka kwa nyanya yake. Alikuwa akienda huko wakati wa likizo za shule hata kabla ya kufikisha umri wa ujana. Kila siku alimwangalia nyanya yake akishona sweta maridadi kwa ajili yake na wanafamilia wengine.

Nyanya yake, ambaye alikuwa ni mwalimu wake, alihisi ni jambo tu la kujifurahisha. Lakini yeye aliona mambo kwa mtazamo tofauti. Kipindi hiko chote, alikuwa akijifunza stadi—ambayo ingekuja kumletea mafanikio makubwa.

Ujuzi wa kujifurahisha unageuka kuwa ajira

Akiwa na umri wa miaka 14 tu, Noah Walakira aliona fursa ya kutumia ujuzi wa kushona aliofundishwa na nyanya yake kuwa kitu chenye faida. Alianza kushona mafulana kwa shule jijini Kampala na kuanzisha shirika la kijamii, Namirembe Sweater Makers. Alipata msaada wa kifedha kupitia mikopo ya benki zinazosaidia biashara ndogo ndogo nchini Uganda.

Mfanyabiashara mwenye mafanikio

Hivi sasa, kampuni hiyo inatengeneza mavazi ya shule kwa zaidi ya shule 45, na pia kwa taasisi nyingine kama makampuni ya usalama na vituo vya mafuta nchini Uganda. Aidha, inahudumia wateja katika nchi kama Rwanda, Sudan Kusini, na Tanzania.

Mbali na kuajiri hadi wafanyakazi 20 wa kijamii, kampuni ya Noah inatengeneza takriban sweta 500 kila mwezi, kila moja ikigharimu takriban dola saba za kimarekani. Kupitia mapato ya biashara hiyo, Noah, pamoja na baadhi ya ndugu zake na baadhi ya wafanyakazi vijana, wameweza kulipa ada za masomo yao.

Sasa, tuangalie jinsi maisha ya kipekee ya Tanya yalivyogeuka kutoka kuwa Mtoto aliye na afya dhaifu kuwa mchezaji maarufu.

Mambo yalipokuwa magumu Tanya hakukata tamaa

Tanya Muzinda alikuwa mtoto mwenye umri wa miaka 11 aliyekuwa bingwa wa Mbio za pikipiki na kuwa uso wa hospitali ya watoto nchini Zimbabwe. Hii ni hadithi ya jinsi jitihada zake na uvumilivu ulivyomfikisha hapa alipo leo, akiwatia moyo watoto wengine kwa kisa chake.10

Alilazimika kuishi maisha ya Upweke kwa sababu ya ugonjwa.

Miezi tisa baada ya Tanya kuzaliwa, kinga ya mwilini mwake ilidhoofika. Alikuwa na upungufu wa kinga mwilini, yaani mwili wake haukuweza kupigana na magonjwa kwa njia ya kawaida, na hivyo alilazimika kuishi mbali na jiji kwa miaka minne ili aweze kuimarika kiafya.

Hakuweza kucheza na watoto wengine kwa hofu ya kupata magonjwa. Hakupaswa kukaa katika maeneo ya umma. Kwa maisha kama haya ya kujitenga, ni rahisi kuelewa kwamba alikuwa na msongo wa mawazo miaka yake ya awali. Nchi nyingi barani Afrika, ni kawaida kwa watoto wengi kukua katika hali ya kukata tamaa kutokana na ukosefu wa kupata huduma salama za matibabu na uangalizi mzuri.

Jitihada za kufanikiwa

Baada ya muda, Tanya alipata nafuu kupitia matibabu na uangalizi wa karibu. Aliweza kurudi mjini na sasa angeweza kuonekana hadharani licha ya hatari zilizokuwepo.

Wengi wanaojitenga kwa muda mrefu huishia kuendelea hivyo kwa sababu wamezoea hali hiyo na huhisi kuwa salama. Lakini Tanya aliamua kujitokeza na kuonyesha kwamba maisha hayapaswi kuongozwa na hofu. Hutakiwi kuruhusu yaliyopita yaamue kesho yako. Hapana, anataka “kuwatia motisha wasichana ulimwenguni.”

Tanya alikuwa na ari kubwa katika mashindano ya mbio za pikipiki. Familia yake ilialikwa kwenye uwanja wa Donnybrook Raceway huko Harare alipokuwa na umri wa miaka mitano na rafiki wa baba yake. Alipenda mbio hizo mara tu baba yake alipomruhusu kujaribu. Akawa msichana wa kwanza kutoka Zimbabwe kushinda mashindano ya mbio za pikipiki za taifa baada ya kumaliza wa pili kwenye mashindano yake ya kwanza. Tangu wakati huo, ameshiriki mashindano hayo kote duniani.

Baada ya muda mfupi, hospitali ya watoto ilimfikia Tanya. Walihitaji mtu wa kuwa sura ya matumaini—mfano wa kuigwa, ambaye angewaonyesha watoto kuwa maisha yanaweza kubadilika. Baba yake aliona hii kuwa nafasi nzuri kwake kusaidia wengine. Kupitia Tanya, watoto wagonjwa wangeweza kuona kwamba hata unapokuwa mgonjwa, umeumia, au unapitia changamoto za kiakili, bado una nafasi ya kufanikisha ndoto zako. Ingawa mabadiliko na mafanikio yanahitaji bidii na uvumilivu, inawezekana siku moja kufanya mambo yanayo kufurahisha, yenye maana unayoyatamani.

Mnamo Disemba 2015, Tanya alikua sura ya mashindano ya pikipiki nchini Zimbabwe11. Amejipatia umaarufu na sasa ni mfano wa matumaini kwa watoto wengi nchini. Sio tena yule mtoto aliyelazimika kukaa ndani bila kucheza na wenzake. Amealikwa kushiriki katika kuhamasisha Mtoto wa Afrika katika sherehe ya siku za kimataifa12, Siku ya Mtoto wa Afrika.13

“Watoto ni mustakabali wa dunia hii. Tunaposherehekea pamoja na mamilioni ya wavulana na wasichana, ningependa kuongea na wazazi wetu, walezi, jamaa, na marafiki kwamba hamtakiwi kuwa sababu ya kuzuia watoto katika ndoto zao. Hebu tuwe na njozi kubwa na mtusaidie kuigundua dunia,14” alisema katika hotuba yake.

Maisha baada ya ugonjwa

Leo, Tanya anawahimiza vijana kuwa ni ndoto zao ambazo zinapaswa kuamua maisha yao, sio mazingira yanayoweza kuwazuia. Anajitokeza katika sherehe za umma kama vile Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike15, akishinda matarajio.

Tanya alitarajiwa kuishi kama mgonjwa na kujificha kwa hofu ya magonjwa yote ambayo angeweza kupata, asiweze kutoka nje ili kutimiza jambo lolote muhimu. Lakini kwa kujitosa katika michezo, alichukua udhibiti wa maisha yake, akikataa kuruhusu matatizo yake kumzuia.

Sasa, watoto wengi wenye magonjwa na ulemavu wa mwili wanamtazama kama mfano16. Anaamini kuwa haupaswi kuishi maisha yako ukiwa na hofu, hata kama hali ni ngumu.

Kustawi licha ya changamoto na vizuizi

Inatia moyo sana kujifunza kile ambacho watu wengine walifanya walipokumbwa na vikwazo na changamoto mbalimbali.

Vijana hawa wa Kiafrika walikuwa na mtazamo chanya, walikuwa na lengo, werevu, na wabunifu. Na kwa kuamua kuendelea mbele na kutokata tamaa, walifaidika si wao wenyewe, bali pia jamii walizotoka.

Wapo wengi ambao sasa wanasaidia kutengeneza simulizi mpya juu ya namna vijana wanaweza kufanya wanapokabiliwa na changamoto za maisha. Je, umewahi kujiuliza kama unaweza kuleta mabadiliko mahali ulipo? Si kwa jambo kubwa mahali fulani, bali kwa changamoto ndogo halisi za jamii yako?

Unaweza kuwa na hofu ya kusimama, kuzungumza, kuwasilisha, kubeba wajibu, kutoa pendekezo, au kushindwa wakati unapojaribu. Lakini kama vijana katika visa hivi, wewe pia, unaweza kuleta mabadiliko popote ulipo.

  1. Chimamanda Ngozi Adichie, “The Danger of a Single Story,” TED Talks, July 2009. []
  2. Andrew Christian, “What Sadio Mane’s Exciting Award Says About Talent And Media Efforts Towards African Sports,” WeeTracker, Jan. 17, 2020 []
  3. Andrew Christian, “What Sadio Mane’s Exciting Award Says About Talent And Media Efforts Towards African Sports,” WeeTracker, Jan. 17, 2020. []
  4. Tuko Kenya, “High school leaver builds own electricity power plant (Amazing Story)Faces of Kenya Documentary, Feb 14, 2018 []
  5. Tuko Kenya, “High school leaver builds own electricity power plant (Amazing Story)Faces of Kenya Documentary, Feb 14, 2018 []
  6. The basket room, 2024, https://www.thebasketroom.com/pages/the-basket-bag []
  7. Ayeshaitu’s story on creating her own opportunities in Ghana,” World Vision, October 18, 2021 []
  8. C. Maya, personal communication, August 2, 2024 []
  9. What was once a pastime is now a business, The Monitor, March 23, 2015, https://www.monitor.co.ug/uganda/lifestyle/reviews-profiles/what-was-once-a-pastime-is-now-a-business-1604900 []
  10. Harris, Chris, “An African Girl with the dream of becoming an International Motocross Athlete,” Andscape, 2013. []
  11. https://www.tanyamuzinda.com/ []
  12. https://www.facebook.com/hashtag/internationdayofthegirlchild []
  13. https://www.facebook.com/watch/?v=512417739240917 []
  14. https://www.facebook.com/tanya.muzinda/videos/today-is-a-special-day-as-we-celebrate-the-world-childrens-day-across-the-globec/512417739240917/ []
  15. https://www.facebook.com/hashtag/internationdayofthegirlchild []
  16. https://andscape.com/wp-content/uploads/2017/08/static1-squarespace.jpg?resize=864,1536 []

Pin It on Pinterest

Share This